Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
Eneo la huduma ya Idara ya DMS litakuwa nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, kwa mwongozo wa Ofisi Kuu ya TAG, idara hii itaweza kufanya kazi nje ya mipaka ya Tanzania. Jina la Idara ni “Idara ya Muziki na Uimbaji”, kwa Kiingereza “Department of Music and Singing” kwa kifupi “DMS”. Andiko la Idara ya DMS litakuwa ni Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli".
Maono ya DMS ni kuwa chombo cha kutafuta, kutunza na kuakisi Uwepo na Utukufu wa Mungu kupitia huduma ya Muziki na Ibada.
Idara ya DMS ipo ili kutunza uhai wa Kanisa kwa kuinua shauku na moyo wa Ibada iliyojaa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu.
Kuchochea vipaji, karama, huduma, na taaluma mbalimbali miongoni mwa wanachama na washirika kwa ujumla ili kuleta ubora na ufanisi katika Ibada.